JINSI YA KUPIKA CHICKEN TANDOORI - (KUKU ALIECHANGANYWA NA VIUNGO)
JINSI YA KUPIKA CHICKEN TANDOORI - (KUKU ALIECHANGANYWA NA VIUNGO)
♦MAHITAJI
1. Kuku mzima 1
2. Kitunguu swaum/tangawizi
3. Maziwa ya mgando 1 kikombe cha chai
4. Curry powder ½ kijiko cha chai
5. Garam masala ½ kijiko cha chai
6. Coriander powder ½ kijiko cha chai
7. Cumin powder ½ kijiko cha chai
8. Chilli powder ½ kijiko cha chai
9. Limao ½
10. Chumvi kiasi
11. Rangi ya chakula nyekundu
12. Mafuta ya kupikia (vegetable oil) vijiko 2 vya chakula
♦JINSI YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
# Katakata kuku katika vipande vya kawaida kisha umuoshe na umkaushe maji kwa kutumia kitchen towel.
# Baada ya hapo muweke katika bakuli kubwa na uanze kutia limao na spice zote kasoro mafuta, yogurt na rangi ya chakula.
# Changanya spice na kuku mpaka vikolee vizuri. Baada ya hapo changanya yogurt na rangi ya chakula pembeni na kisha umwagie katika kuku na uchanganye tena vizuri.
# Baada ya hapo malizia kwa kutia mafuta na uchanganye vizuri kisha funika na uweke katika friji kwa muda wa masaa 3 ili kuku aingie viungo.
# Baada ya hapo muoke kuku wako katika oven kwa muda wa nusu saa katika moto wa 200°C.Baada ya hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment