MTUKUTU ALBERT SPAGGIARI MHALIFU ALIYESHANGAZA DUNIA KWA USTADI WAKE (SEHEMU YA KWANZA)
Katika ufanikiwaji wa jambo lolote ni lazima ujitoe sadaka katika kuhakikisha linafanikiwa, ueledi na nidhamu lazima itawale kwa kiasi kikubwa ili kufikia malengo. Hata kwenye kufanikisha uhalifu nidhamu na ueledi ni nguzo za kuzingatia. Leo tutaenda kumuona huyu jamaa aliyeweza kuiba moja ya benki kubwa nchini ufaransa.
ALBERT SPAGGIARI ni kijana aliyezaliwa katika mji wa LARAGNE-MONTEGLIN unaopatikana katika safu za milima ALPES tarehe 14 disemba 1932, pia alijulikana kwa jina lingine liitwalo BERT[nick name]. Spaggiari akiwa bado bwana mdogo alipata mchumba ambaye alimpenda sana na hakupenda yeye kuonekana mwanaume suruali na ukizingatia alikuwa ametoka katika familia ya hali ya kawaida, kwani mama yake alikuwa na stoo ya kuuzia nguo za ndani[chupi] katika mji wa HYERES ambapo ndipo alipokulia bwana SPAGGIARI. Na ikumbukwe alilelewa na mama yake pekee.
Kutokana na kutaka kumfurahisha mchumba wake bwana mdogo alijaribu kuvunja na kuiba almasi ili mradi aende kumpa mchumba wake kama zawadi ila mwishoe hakufanikiwa kwani alikamatwa na polisi wakati akijaribu kufanya tukio. Na kumfanya ashtakiwe na kufungwa jela.
Katika kifungo chake bwana spaggiari alikubaliana na mamlaka ya jeshi kuwa ni lazima atashirika katika vita ya INDOCHINA kusaidia ufaransa, na aliambiwa atapewa mafunzo ya kuweza kuwa sehemu ya kikosi cha maparashuti [Wanajeshi wanaoshuka kwa maparashuti]. Baada ya kutoka kifungoni na kutumikia jeshi, aliamua kujihusisha na mambo ya upigaji na uhariri wa picha, mpaka kufikia 1976 aliweza kumilika studio yake mwenyewe katika mji wa NICE nchini ufaransa.
Ila baada ya muda mfupi akaanza kuboreka kwa kuwa na maisha ya kati na hivyo aliona namna pekee ya kuongeza kipato ni kuweza kujiongeza na ndipo akaanza kuwa mbunifu na mwanamitindo katika mji wa NICE.
Baada ya kujiongeza katika taaluma zingine hizo ila bado hazikumuingizia kama anavyotaka na aliona inamchelewesha, ndipo alipoamua kuangalia upande wa pili na kukumbuka kuwa alishawahi kujaribu kuiba ila hakufanikiwa. Akajaribu kuangalia alikosea wapi mpaka akakamtwa.
INAENDELEA.....!!!!
Subscribe your email address now to get the latest articles from us
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment